Kauli hiyo imekuja muda mfupi
wakati waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu -Tamisemi Hawa Ghasia wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa madreva
watakaokuwa wakiendesha mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam
Amesema kuwa KAMERA hizo
zitafungwa katika mabasi kufuatilia mienendo ya abiria pamoja na dereva wa gari
husika ili kuweza kuona namna anavyoendesha na wale wenye tabia za kuchora
chora City za mabasi na mambo mengine.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Said Meck Sadick amesema ipo haja ya kampuni ya wazawa ya UDA-RT iliyopewa
dhamana ya kuendesha mradi huo kuonyesha kwa vitendo kuwa inaweza licha ya
kuwepo propaganda kuwa mradi huo ulitakiwa kuendeshwa na makampuni ya kutoka
nje ya nchi.
Baadhi ya wakazi wa DSM wamesema
wanatumai huenda kwa utaratibu huo ukapungua licha kwamba si sehemu zote huduma
hiyo itakapo fika ila angalau inaonyesha taswira.
Kampuni
ya ubia ya UDART kwa kushirikiana na wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART)
imeanza leo kuendesha mafunzo kwa madereva wake kabla ya huduma ya usafiri
kuanza rasmi Oktoba Mwaka huu.
Mafunzo hayo yalioanza leo kwa madereva hao wa mabasi,yalianza na mabasi mawili ya mwendo kasi kutoka Kimara hadi Kivukoni kwa abiria wakisafiri bure njia ambayo mradi huo utaanza kufanya kazi kwa majaribio.
Mafunzo hayo yalioanza leo kwa madereva hao wa mabasi,yalianza na mabasi mawili ya mwendo kasi kutoka Kimara hadi Kivukoni kwa abiria wakisafiri bure njia ambayo mradi huo utaanza kufanya kazi kwa majaribio.
0 comments:
Post a Comment