Watu 37 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kuzama kando ya Libya kwenye Bahari ya Kati ikiwa ajali ya pili kando ya Libya ndani ya siku chache kusababisha maafa makubwa.
Alhamisi iliyopita watu zaidi ya 200 wamekufa kando ya Libya wakati mashua mbili zilizokuwa na watu wapatao 500 kuzama.
Tukio la sasa limeelezwa na Chama cha Mwezi Mwekundi cha Tripoli na kwamba ajali hiyo ilitokea Khoms kilomita 100 mashariki ya Tripoli lakini hayakutolewa maelezo zaidi.
Mpaka sasa mwaka huu wahamiaji 2,500 waliokuwa wanajarubi kwenda Ulaya wamekufa maji ikilinganishwa na 3,500 kwa mwaka mzima uliopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment