Image
Image

Watoto 163 waliokuwa wanashikiliwa na kikundi cha Afrika ya kati waachiliwa huru.

Kikundi kimoja cha wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kimewaachia watoto 163 waliokuwa wanashikiliwa na kikundi hicho na hivyo kufikisha kuachiliwa kwa watoto 645 waliokuwa wanashikiliwa na vikundi vya wapiganaji.
Watoto hao wakiwemo wasichana watano walikabidhiwa kwa mamlaka husika wakati wa hafla iliyowezesha na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyofanyika mji wa kaskazini wa Batangafo.
Watoto hao waliachiliwa na kikundi cha wanamgambo wa Kikristo cha anti-Balaka ambacho bado kinapambana na wapiganaji wa mseto wa zamani wa waasi wa SELEKA wenye Waislamu wengi.
Jamhuri ya Afrika ya Kati yenye vijana wapatao Elfu-10 wanaotumiwa kama askari na makundi ya wapiganaji ilitumbukia kwenye machafuko ya kidini mwaka 2013.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment