Na.Sadick Juma,Mtwara.
Mgombea
mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia ukawa Mh. Juma Duni
Haji amesema hakuna sababu kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara
na lindi kuendelea kupunjwa bei ya zao hilo na serikali ya chama cha mapinduzi
kwa kulipwa shilingi mia sita badala ya bei dira ya shilingi elfu moja
iliyotangzwa msimu wa 2014/2015 na kuwahaidi watanzania kuwa UKAWA ikiingia
madarakani itafuta mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa ukitumika
kuwanyonya wakulima wa mazao mbalimbali nchini.
Akizungumza
na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mtwara waliohudhuria mkutano huo wa kampeni za
urais za vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi – UKAWA,zilizofanyika
katika uwanja wa mashujaa mjini MTWARA – mgombea mwenza huyo amesema ikiwa
watanzania wataipa ridhaa UKAWA ya kuongoza dola, watahakikisha wanafuta mfumo
wa stakabadhi ghalani na kuboreshabei ikiingia madararakani.
Mapema
akiwahutubia wananchi wa mji wa Newala,Mh.Juma Duni Haji pamoja na viongozi
wengine wa kitaifa wa vyama vya NCCR – Mageuzi,chama cha wananchi ( CUF )
pamoja na CHADEMA, wamesema kuwa licha ya gesi kugunduliwa mkoani Mtwara,neema
hiyo imegeuka kuwa mateso kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo huku ufafanuzi
kuhusu kashfa ya RICHMOND ambayo imekuwa ikihusishwa na waziri mkuu mstaafu Mh.
Edward Lowassa ambaye kwa sasa ni mgombea urais wa CHADEMA kupitia ukawa
ukizidi kuwekwa bayana.
Mgombea mweza wa UKAWA anazungumza hapa*Like Page na kuwa wa kwanza kusoma taarifa zetu .
Mgombea mweza wa UKAWA anazungumza hapa*Like Page na kuwa wa kwanza kusoma taarifa zetu .
0 comments:
Post a Comment