Wananchi wa eneo la misusugu mkoani Pwani wamefunga
barabara baada ya wanafunzi wa kike 3 kudaiwa kugongwa na gari la Jeshi la Polisi
mkoani humo na kufariki dunia,hivyo
kusababisha Wazazi,Walezi na Wanafunzi katika eneo hilo kufunga barabara kwa
kuandamana.
Taarifa toka eneo la tukio zinaeleza kwamba hali ni
mbaya katika eneo hilo kutokana na msongamano mkubwa wa magari kuzuiliwa na
wananchi hao wenye hasira kali na polisi wanatumia mabomu kuwatawanya
waandamanaji hao.
Taarifa Zaidi itawajia muda si Mrefu.
0 comments:
Post a Comment