Wananchi wakiwa wamejipanga
msururu kila mmoja kutaka kuona kilichotokea baada ya gari hizo kugongana na
kusababisha ajali(Picha na Maktaba).
Pamoja jitihada za jeshi la Polisi Mkoani Kagera za kubuni mikakati ya kukabiliana na ajali za barabarani kwa kushirikiana na idara nyingine za serikali na wadau mbalimbali bado mkoa huo unaendelea kukabiliwa na ongezeko la ajali ambazo hutokea na wakati mwingine husababisha vifo na majeruhi.Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo katika Mkoa wa Kagera yamefanyika Wilayani Misenyi, Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo, WILLIAM MKONDA wakati akitoa takwimu za hali ya ajali na mambo yanayosababisha ajali katika mkoa huo.
Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu idadi ya ajali zilizotokea Mkoani Kagera na kusababisha vifo na majeruhi kuwa imeongezeka ikilinganishwa na ajali zilizotokea mwaka jana katika kipindi hicho.
Kwa upande wake, OBEDI ILOMO, Katibu Tawala wa Wilaya ya Misenyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani kutekeleza majukumua yao kwa uadilifu.
0 comments:
Post a Comment