MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seleman Jabil amefafanua
namna alivyopewa jina la Msaga Sumu ambalo sasa linampa umaarufu mkubwa.
Msaga Sumu alisema amepewa jina hilo
kutokana na biashara aliyokuwa anaifanya ya kuuza mitumba ambapo anasema
kila alipokuwa anafungua mzigo wa nguo alizokuwa anauza alikuwa
anapendelea kutoa nguo nzuri na kuziita sumu.
“Hii nguo sumu yaani kila nikifungua mzigo nikikutana na kitu kizuri
ni lazima nikiite hivyo hivyo na ndio mwanzo wa kupewa jina la Msaga
Sumu ambalo linanipa umaarufu hadi sasa katika tasnia ya muziki
ninaoufanya,” alisema.
Katika hatua nyingine, Msaga Sumu alizungumzia muziki anaoufanya ambapo aliweka wazi kuwa kazi zake zinapendwa hadi na mashehe.
“Namshukuru Mungu kazi zangu hazibagui umri zinapendwa na kila mtu
chakushangaza zaidi hadi mashehe wanazipenda kwasababu kuna siku
nilikuwa nafanya tamasha Mabibo kuna Shehe alinifuta na kuniambia
anapenda sana kazi zangu,” alisema
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment