Anselme Seka Yapo alikuwa kiongozi wa kikosi cha ulinzi kilichokuwa
kikimlindia usalama mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.
Seka Yapo alihukumiwa Jumanne na mahakama hiyo pomoja na maafisa
wengine 7 walioshitakiwa uhalifu uliotendeka baada ya uchaguzi
uliofanyika nchini humo mwaka 2010.
Seka Yapo amehukumiwa kifungo hicho
baada ya kukutwa na hatia ya kumuua dereva wa zamani wa waziri wa haki za
binadamu Joel N’Guessan mwaka 2011.
Kamishna Ange Kessi
alifahamisha kuwa iwapo Yapo, mtu katili ambae aliewauwa watu wasiokuwana hatia
akisalia uraiani basi Ivory Coast haitokuwa na amani.
0 comments:
Post a Comment