Afisa mkuu wa AU alisema kwamba kamati yao inapanga kukutana na makundi ya waasi ya Sudan kwa lengo la kuwashauri kuhusu mazungumzo ya masuala ya kitaifa.
Mkuu wa kamati ya AUHIP Thabo Mbeki, alisema kuwa wataandaa mkutano na wawakilishi wa makundi ya waasi ya Sudan ili kuwashawishi kufanya mazungumzo na serikali ya Khartoum.
Siku ya Jumatatu, Makamu wa rais wa kwanza wa Sudan Bakri Hassan Saleh, alitoa maelezo kwa vyombo vya habari na kusema kuwa hawatoruhusu mazungumzo kufanyika nje.
Saleh alitilia mkazo suala hilo na kuhimiza makundi ya waasi kushiriki kwenye mazungumzo ya Khartoum.
Mnamo mwezi Januari mwaka 2014, rais wa Sudan Omar al-Bashir alitoa wito kwa vyama vya upinzani na makundi ya waasi kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili kutatua mizozo nchini.
0 comments:
Post a Comment