Hii ndio Orodha ya nchi zinazovutia wawekezaji wa kigeni barani Afrika.
Benki moja ya uwekezaji nchini Afrika Kusini imechapisha orodha ya nchi 10 za kwanza zinazovutia wawekezaji wengi zaidi wa kigeni barani Afrika.
Afrika Kusini inaongoza orodha hiyo huku ikifuatia na Nigeria, Ghana, Morocco, Tunisia, Misri, Ethiopia, Algeria, Rwanda na Tanzania.
Orodha hiyo ilichapishwa baada ya utafiti kufanyika kwa kuzingatia viwango vya soko la uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa na ukuwaji wa uchumi.
Nchi hizo zilizoingia kwenye orodha ya 10 bora, zimeonyesha ufanisi na kuchangia pakubwa katika soko la biashara za kimataifa.
Nchi ya Rwanda ambayo imefanikiwa kujumuishwa kwenye orodha hiyo, pia iliwahi kushikilia nafasi ya 46 kati ya nchi 189 kote ulimwenguni katika orodha ya benki ya dunia ya mwaka 2015 kwa ukuwaji wa kibiashara.
0 comments:
Post a Comment