Rais Yoweri Museveni (pichani) wa nchi hiyo anatarajiwa kulihutubia
Bunge hilo Agosti 12 na litaongozwa na Spika wake, Daniel Kidega.
Kwa mujibu wa msemaji mwandamizi wa EALA, Bobi Odiko, ajenda
katika kikao hicho cha wiki mbili itakuwa kujadili miswada muhimu
itakayowasilishwa na kusomwa mmoja kwa mara ya pili na mwingine kwa mara
ya tatu.
Aliitaja miswada hiyo kuwa ni Muswada wa Sheria ya Elekroniki wa 2014 na Muswada wa Sheria ya Ubunifu wa Viwanda wa 2015.
Alisema Muswada wa Elektroniki unataka kuweka mazingira ya kutumia
teknolojia hiyo katika shughuli za kibiashara katika dunia ya sasa.
Kwa mujibu wa Odiko, muswada huo pia unataka kukuza teknolojia
katika matumizi ya mawasiliano, shughuli za Bunge, kuendeleza usalama,
kulinda na kuweka mazingira mazuri ya walaji, biashara na serikali za
nchi wanachama.
Alisema EALA tayari imekwishapokea maoni mbalimbali ya wadau kuhusu muswada huo.
Akizungumzia Muswada wa Sheia ya Ubunifu na Viwanda wa 2015, ambao
ulisomwa kwa mara ya kwanza Januari mwaka huu, alisema madhumuni yake
makubwa ni kukuza ubunifu na viwanda katika nchi wanachama.
“Muswada unaka kuanzisha Baraza la Ubunifu na Viwanda ambalo
litaweka mazingira mazuri ya kukuza na kuhamasisha ubunifu miongoni mwa
wananchi,” alisema.
Odiko aliongeza kusema kuwa, baraza hilo litakapoanzishwa
litahakikisha kuna kuwa na mafunzo maalum yenye viwango vya ubora na
ujuzi na maendeleo ya ubunifu na kuanzisha sera na mikakati ya
kuziwezesha nchi wanachama kutumia vipaji vya vijana.
0 comments:
Post a Comment