Image
Image

Maandalizi Ligi, ukarabati viwanja unaendelea -TFF.


Shirikisho la Soka nchini TFF limesema wameshirikiana na Bodi ya Ligi kupitia idara ya ufundi na mashindano katika ukaguzi wa viwanja vyote vitakavyotumika katika michuano ya Ligi kuu, Daraja la kwanza na Daraja la Pili.
Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, katika ukaguzi huo wamekuta baadhi ya viwanja vinatakiwa marekebisho na wahusika wameshapewa maelekezo kwa ajili ya kufanyia ukarabati viwanja hiyo.
Kizuguto amesema, wanaamini wahusika watafanya marekebisho kabla ya kuanza kwa Ligi hiyo ambapo kabla ya kuanzaviwanja vyote vitakuwa vimekamilika ili kujihakikishia utumiaji wa viwanja hivyo.
Kizuguto amesema, watakapotoa ratiba pia watazingatia viwanja vyote vipo katika hali bora inayokidhi kuchezewa kwa Ligi hivyo anaamini kwa vichache vilivyokuwa na mapungufu anaamini vitafanyiwa marekebisho mapema kabla ya kutoka kwa ratiba ambapo wakaguzi watapita mara ya mwisho kabla ya kutoa ratiba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment