Image
Image

Umoja wa wasanii nchini wamtangaza JK kuwa shujaa wa sanaa ya muziki nchini Tanzania.


Umoja wa wasanii nchini Tanzania umemtangaza rais Jakaya kikwete kuwa shujaa wa sanaa ya muziki nchini katika hafla maalumu ya kumuaga na kumshukuru kwa namna ambavyo ameweza kuwasaidia katika sekta hiyo tangu alipo ingia madarakani hadi hivi leo ambapo anakaribia kufikia ukingoni mwa uongozi wake kama rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Hafla hiyo ya kumuaga imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa  na viongozi mbali mbali wa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na hivyo Rais Kikwete akatumia wasaa huo kumtambulisha Mgombea urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya wasanii hao.

Rais kikwete amesema kuwa kazi ya sanaa ni ya kuheshimiwa kama kazi nyingine kwani sanaa si uhuni kama wengine wanavyo dhani kwakuwa muziki ni sehemu ya maisha ya mwanadamu hivyo inasikitisha kuona msanii akitumia kipaji chake,tungo zake kuwa tumbuiza watu nahivyo kuondoka jukwaani pasipo kuwa na pesa inayoweza kumkidhi nijambo ambalo halileti picha nzuri kwa taifa,Huku akitolea mfano Beyonce kuwa binti mdogo lakini muziki unamlipa vizuri na anafurahia sanaa yake.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwahakikishia wasani kuwa hata atakapo maliza kipindi cha uongozi wake ataendelea kuwatumikia kwa kuwa anaupenda mziki unamliwaza hata pale alipokuwa anamawazo hivyo anajua thamani ya mziki na sanaa kiujmla huku akimtolea mfano JB kuwa inafika wakati kapumzika anaangalia filamu yake,hivyo anawaahidi kuwa yeye atakuwa mlezi wa wasanii na sanaa kiujumla.

Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa wasanii ni watu muhimu ambao kazi zao zinapaswa kulindwana kuheshimiwa  ili ziwanufaishe kama ilivyo kwa wasanii wengine duniani na kuahidi kuendelea kusaidia juhudi za kuwafanya wasanii waishi maisha yaliyo bora kwa kupata kipato kinacholingana na kazi zao hata akishastaafu nafasi yake ya urais.
Mapema wasanii walimtawaza Rais Kikwete kuwa Shujaa wao, na kumtunuku picha maalum iliyonakshiwa karibu majina ya wasanii wote nchini, Picha hiyo alikabidhiwa na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nikki wa Pili ambaye kabla ya tukio hilo, alieleza jinsi tasnia ya sanaa, inavyochangia pato la taifa na changamoto zinazowakabili wasanii.

Rais Kikwete amesema kuwa wakati maswala mbali mbali ya wasanii yakishughulikiwa ni wakati sasa kuwa kila kituo cha Radio kitakacho cheza wimbo wa msanii husika kitaweza kumlipa kwani hata nchi za nje wanafanya hivyo,kwa hiyo kwa Tanzania haitakuwa ajabu kwani wenye vipindi hivyo vya burudani wanakuwa wanawatu wanao wadhamini  hivyo itasaidia kukuza sanaa nchini.

Katika hafla hiyo, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walichangamsha ukumbi, baada ya kupanda jukwaani na kuzicharaza ala za muziki kwa umahiri mkubwa.

Baadhi ya wasanii wengine waliotumbuiza ni Farid Kubanda (Fid Q), Shakila, Rud, Jose Mara.
 Rais Jakaya Kikwete akiingia katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kuhudhuria chakula cha jioni, kilichoadaliwa kwa ajili ya Rais Kuagana na wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini, jana usiku. Pamoja naye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
                                                    HABARI KATIKA PICHA
Rais Jakaya Kikwete na viongozi aliofuatana nao wakiwa wamewasili ukumbini na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii waliohudhuria ukumbini.
                              Kassim Mponda akiwa na wenzake maarufu.
                                  Mzee Kingi Kikii akiwa na wenzake maarufu.
                            Rais Kikwete  akimsalimia Mzee Yusuf kwa furaha.
                                            Akimsalimia pia mke wa Mzee Yussuf.
                      Mzee Yussuf akapata fursa ya kuteta jambo Rais Kikwete.
       Wasanii wakijipiga picha kwa simu na Rais Kikwete wakati akiwasalimia.
                        Rais Kikwete akiwasalimia kwenye meza ya Kina Baba Zoro.
Rais Kikwete alifurahi kiasi cha kukumbatiana na baadhi ya wasanii, kama alivyofanya hapa.. 
        Rais Kikwete akiendelea kusalimia wasanii meza moja baada ya nyingine.
            Akafika hadi meza aliykuwepo Madam Rita wa Bongo Star Search.
          Nao wakapata fursa ya kujipiga picha na Rais kwa kutumia simu yao.
                                   Rais akafika hadi kwa Juma Kaseja.
                                                    Salam zikaendelea .
Rais Kikwete akajitahidi kusalimia kila mmoja na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii wakiwa kwenye meza zao.
                               Wasanii wakiwa wameketi kwa utulivu mezani.
                                            Bi Shakila akiwa na mwenzake.
                                             Fid Q akiwa ndani ya nyumba.
                   Wengine wakiwa katika nyuso za kutafakari hali ya mambo.
                                           Wengine wakiendelea na vinywaji.
                                 Wasanii wakijichanganya bila kujali fani zao.
                                      Ally Chocky (kushoto) ndani ya nyumba.
           Diamond Platinum akisalimia wenzake baada ya kuingia ukumbini.
                                       Jay B (kushoto) pia ndani ya nyumba.
Baadhi ya wakurugenzi wa vyombo vya habari wakiwa ndani ya nyumba. hapo kuna Benny Kissaka (kushoto) na kulia ni Danny Chongolo.
                                                     Rey naye ukumbini.
                       Mzee Yussuf na mkewe wakiwa ndani ya nyumba.
                                          Kina Juma Kaseja ndani ya nyumba.
                            Msanii Rubby akiimba wimbo maalum wa kuisifu Tanzanaia.
                                        Fid Q akiimba kutumbuiza ukumbini.
     Jose Mara akiimba wimbo wa Mbaraka Mwishehe wa kuisifia Morogoro.
Diamond akitoa tamko kuhusu tasnia ya Sanaa, alisema, kabla ya umaarufu aliwahi kudandia kampeni za CCM kutoka Mwanza hadi Dar, hadi akatambuliwa.
                                 Rais Kikwete uso kwa uso na Msanii na Msanii King Majuto.
               Bi Shakira akiimba wimbo Macho yanacheka Moyo unalia.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akizicharaza tumba, huku Nape akicharaza Bess.
                                                 Recho akiimba wimbo wa Sikinde.
Msanii akimtunza Dk. Magufuli Dola za marekani baada ya kuvutiwa anavyocharaza tumba.
                  Jay B na Mwana FA wakiwa wamekaribishwa kuketi meza kuu.
            Bushoke akiimba wimbo wake wa maarufu wa kunyanywaswa na mke.
           Shughuli hiyo ikamfikisha Hussein Bashe katikati ya Nape na Kinana.
                                                 Kinana akimshauri jambo Bashe.
                                        Rais Kikwete akipata picha na Fid Q
                 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akisakata mzuziki na Madam Rita
                               Rais Kikwete akisakata muziki katikati ya wasanii.
 Nikki wa pili akitoa maelezo kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete picha maalum
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa picha maalum yenye majina ya wasanii karibu wote, kutoka kwa Nikki wa Pili. Kulia ni Fid Q.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment