Timu ya Manchester United ilifungua
msimu mpya wa EPL kwa mechi kali dhidi ya Tottenham
Hotspur iliyochezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Old Trafford, na
kuondoka na pointi 3 baada ya ushindi wa 1 – 0.
Siku hiyo hiyo, Chelsea nayo
iliponea chupu chupu uwanjani Stamford Bridge baada ya kutoa
sare ya 2 – 2 na Swansea City katika mechi waliyolazimika
kutamatisha na wachezaji 10. Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois,
alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 52 baada ya kumtendea madhambi
msahmbuliaji wa Swansea City, Gomis.
Katika ratiba ya siku ya Jumapili, mabingwa wa taji
la FA Cup na Community Shield Arsenal, walijipata matatani
baada ya kuaibishwa mbele ya mashabiki na West Ham United. Arsenal
walipokea kichapo cha bao 2 – 0 na kuambulia patupu bila pointi yoyote.
Mechi ya mwisho ya siku ya Jumapili ilichezwa kati ya Stoke City
na Liverpool ambapo kiungo wa kati Philippe Coutinho aliiokoa
Liverpool katika dakika za mwisho na kuiletea pointi 3 baada ya
ushindi wa 1 – 0.Timu ya Manchester City itajitosa uwanjani kupambana na West Bromwich Albion leo usiku katika mechi itakayotamatisha wiki ya kwanza ya EPL.
Matokeo kamili ya mechi za EPL zilizochezwa ni kama ifuatavyo;
Manchester United 1 - 0 Tottenham Hotspur
Bournemouth 0 - 1 Aston Villa
Everton 2 - 2 Watford
Leicester City 4 - 2 Sunderland
Norwich City 1 - 3 Crystal Palace
Chelsea 2 - 2 Swansea City
Arsenal 0 - 2 West Ham United
Newcastle United 2 - 2 Southampton
Stoke City 0 - 1 Liverpool
0 comments:
Post a Comment