Na Bryceson Mathias, Ruaha-Kilosa.
BAADA
ya kuwepo Mizengwe na Mamluki toka nje ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha Kilombero kutaka kuvuruga Uchaguzi wa
Mgombea wa Udiwani, hatimae Mshindi wa Matokeo ya Mnyukano wa Uchaguzi
huo, sasa yamewekwa Hadharani.
Akizungumza na Tanzania Daima,
Katibu wa Chadema Kata ya Ruaha, Joramu Zacharia , almtaja , Isaack
Maliwa, kuwa ndiye Mshindi kwa kujikusanyia Kura (43), akiwashinda,
George Banda (40), Ally Mponda (6), Mathias Luambano (4), Kilango Mshana
(0) na Manji Mbando (0).
Uchaguzi huo uliwahusisha Wagombea Sita
(6), ambapo wapiga kura walikuwa 95, wakiwa ni Wajumbe toka katika
Vijiji Vinne (4) vya, Ruaha, Simbalembende, Nyanvisi na Kising’a,
vikiwakilishwa na Wenyeviti wa Vitongoji na wajumbe wa Baraza la Kata ya
Ruaha.
Akiwashukuru Wajumbe Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya
Kilosa, Kamanda Libenaga, alisema Kata ya Ruaha ndiyo yenye Chachu ya
Mabadiliko, ambayo kwa sehemu kubwa itasaidia kupata Ushindi wa Ubunge
wa Jimbo la Mikuni kwa sababu ina watu wengi.
Mshindi wa Uchaguzi
huo, Maliwa, aliwashukuru Wapiga Kura wote, huku akikiri kuwa ulikuwa
na ushindani Mkubwa, ambapo alisema kama Chama kitaridhia na kumpitisha
apeperushe Bendera ya Chadema katika Uchaguzi huo, atashirikiana na
Wagombea wote kuhakikisha Wanapata Ushindi wa Kata ya Ruah na Jimbo la
Mikumi.
Hata hivyo, Maliwa aliahidi, “Kama Chadema kitampisha
Kugombea Uchaguzi wa Kata ya Ruaha, Mshindani wake aliyemfuatia, Banda,
atakuwa Kampeni Meneja wake, ili kwa Umoja na Mshikamano wao, ulete
Mabadiliko Makubwa zaidi”.alisema Maliwa.
Kauli hiyo iliungwa
Mkono na Mshindani wake Banda, ambaye bila Kinyongo huku wakikumbatiana,
alikubali kushirikiana na Mshindi huyo, endapo atapitishwa na Chama
chao, ambapo Wajumbe na Wasimamizi wa Uchaguzi huo, walipendezwa na
Mshikamano na Umoja ulioonyeshwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment