Image
Image

Mlipuko wa surua umeua watu 315 waambukiza 20,000 Kongo.

Mlipuko wa surua umeua watu 315 na wengine zaidi ya 20,000 wamepata ugonjwa huo katika shaba la Katanga huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imesema inaelekea takwimu za vifo zaidi hazikuweza kupatikana kutokana na ugumu wa kuyafikia maeneo ya mbali.
Ofisi hiyo imesema kiasi cha dola milioni 2.4 kitahitajika ya kuandaa chanjo na tiba kwa
walioambukizwa ugonjwa huo katika jimbo hilo la kusini-mashariki mwa Kongo.
Jimbo la shaba la Katanga ni sugu kwa milipuko ya surua na katika mlipuko wa mwaka
2010/2011 zaidi ya watu 1,000 walikufa na wengine 77,000 kuambukizwa ugonjwa huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment