Pinda alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga Mafunzo ya Uongozi
Daraja la kwanza, kozi ya 21 kwa askari 711 wa Jeshi la Magereza
yaliyomalizika katika Chuo cha Magereza Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa sasa linamiliki ardhi kubwa
inayofaa kwa kilimo ambayo inafikia hekta 72,752, lakini eneo
linalotumika kwa kilimo ni hekta 3,169 pekee.
“Ardhi hii ni rasilimali kubwa kwani, mkiitumia vizuri pamoja na
rasilimali watu ambayo pia mnayo ya kutosha, naamini kuwa mnaweza
kuzalisha chakula cha kujitolesheleza nyie wenyewe kama Jeshi na pia
kusaidia majeshi mengine kwa chakula nchini,” alisema Pinda.
Mahitaji ya chakula cha magereza nchini kwa sasa ni wastani wa tani
8,450.5 za mahindi, tani 1,976 za mpunga na tani 1,308.7 za maharage.
Pinda alisema kuwa kwa sasa Jeshi la Magereza nchini linazalisha
wastani wa tani 2,051.1 za mahindi ambazo ni sawa na asilimia 24 ya
mahitaji, tani 317.7 za mpunga sawa na asilimia 16 na tani 14.7 za
maharage ambazo pia ni sawa na asilimia 1.1 ya mahitaji yote.
Alisema kuwa kutokana na Jeshi hilo kuwa na rasilimali kubwa ya
ardhi na watu, halipaswi kuendelea kutegemea bajeti ya Serikali kwa
mahitaji ya chakula na badala yake umefika wakati wa kujitegemea.
0 comments:
Post a Comment