Serikali imekiri vitendo vya ufanikishwaji wa mauji
na uporaji wa silaha Katika vituo
mbalimbali vya polisi hapa nchini vinasababishwa na uzembe wa Askari
polisi kutokua makini wawapo kazini
,ulevi na kukaribisha watu Wasiowajua undani wao wakiwa wamebeba silaha.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.pereira
ame silima ameyasema hayo Wakati akifunga mafunzo ya awali ya jeshi la polisi
na uhamiaji katika chuo Cha taaluma ya Polisi Moshi(mpa).
Amesema askari polisi wengi wamejisahau wawapo
kazini kutokana na baadhi Yao kulala ,kutowatilia shaka watu wanaoingia katika
vituo vya polisi ,kutofanya ukaguzi jambo ambalo linasababisha askari kuvamiwa
na wahalifu Kiholela.
Kwa upande wake naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini
abrahaman kaniki Amepiga marufuku kwa askari wa jeshi la polisi kujihusisha na
ushabiki,itikadi za kisiasa na wagombea wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Naye mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi moshi(mpa)afande
matanga mbushi Amesema jumla ya askari polisi na uhamiaji 126 kati 3610
waliojiunga na Jeshi hilo waliachishwa mafunzo kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo utovu Wa nidhamu.
Baadhi ya viongozi wa dini waliotoa nasaha zao
wamesema tatizo la rushwa na Ukosefu wa maadili kwa watumishi wa uuma
umesababisha wananchi wengi kukosa Haki zao zao za msingi.
Haya ndio maneno ya Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Pereira Ame Silimaakisimulia #BofyaHapachini Like Page yetu kupata Habari zaidi.
Haya ndio maneno ya Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Pereira Ame Silimaakisimulia #BofyaHapachini Like Page yetu kupata Habari zaidi.
0 comments:
Post a Comment