Na Princess Asia, DAR ES SALAAM.
BAO
pekee la Awadh Juma Issa dakika ya 89, limeipa Simba SC ushindi wa 1-0
dhidi ya SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo wa kuhitimisha tamasha la Simba Day, Awadh alifunga bao hilo
baada ya kuuwahi mpira uliorudi kufuatia kupanguliwa na kipa Stephen
Odongo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa SC Villa.
Haukuwa
ushindi mwepesi kwa Simba SC, kwani SC Villa walionekana kuwa wapinzani
wagumu kwao tangu mwanzo, licha ya kucheza pungufu tangu dakika ya 44
baada ya Yoseri Waibi kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu
Ibrahim Hajib.
Simba
SC ilianza kucheza soka ya kuvutia na kusisimua mashabiki wake kipindi
cha pili, baada ya kocha Muingereza Dylan Kerr kufanya mabadiliko
kadhaa.
Waliobadili
mchezo ni beki wa kushoto, Mrundi Emery Nimubona ambaye alikuwa anatia
krosi maridadi zilizozua kizazaa langoni mwa wapinzani na Mwinyi
Kazimoto ambaye alikwenda kuiongoza timu vizuri.
Kipa
Vincent Angban kutoka Ivory Coast alikuwa kivutio kutokana na kulinda
vizuri lango la Simba, ikiwa ni pamoja na kuokoa michomo kadhaa ya
hatari.
Mshambuliaji
Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyewahi kucheza kwa mahasimu, Yanga SC
alikuwa mwiba kwa mabeki wa SC Villa, lakini alishindwa kufanya kitu
kimoja tu- kutumbukiza mpira nyavuni.
Pamoja
na ushindi huo, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, kocha Kerr ana kazi nzito ya kufanya ili Simba SC ifikie katika
ubora wa kuweza kushindania taji dhidi ya Azam na Yanga.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy/Emery Nimubona
dk62, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Samih Hajji Nuhu dk75, Hassan
Isihaka, Juuko Murushid, Justuce Majabvi, Said Ndemla, Ibrahim
Hajib/Simon Sserunkuma dk46, Hamisi Kiiza/Danny Lyanga dk83, Mussa
Mgosi/Boniphace Maganga dk84 na Peter Mwalyanzi/Mwinyi Kazimoto dk46.
SC
Villa; Stephen Odongo, Misi Katende,Yoseri Waibi, Henry Katongole, Paul
Mbowa, Jonathan Mugabi, Godfrey Lwesibawa/Eturude Abel dk73, Martin
Kiiza, Tokko Fahad/Kasumba Umaru dk66 na Robert Achema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment