MSANII wa Bongo Movie anayetambulika kwa jina la Aunty Ezekiel
amewajia juu mashabiki wake wanaomuongelea vibaya mtoto aliyezaa na
mnenguaji wa Diamond Platnumz, Mozee Iyobo.
Aunty Ezekiel aliandika katika mtandao wa jamii kwamba amesikitishwa
na namna baadhi ya mashabiki wake wanavyong’ang’ania aweke picha ya
mtoto wake anayetambulika kwa jina la Cookie.
“Kuweka uso wa mwanangu mtandaoni ni hiari yangu, msilazimishe,
mwanangu ni mweusi sana au ana chongo siwezi kumuanika hadharani, mimi
ndiye najua utamu na uchungu wake, ningetaka kuzaa mtoto mweupe ningezaa
na mzungu,’’ aliandika Aunty Ezekiel.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment