Akihojiwa katika Redio Sauti ya Amerika (VOA) jana, Mwanasheria wa
Chadema, Tundu Lissu, alihoji sababu za Dk. Slaa kuibuka sasa na kusema
Lowassa hakuweka wazi masuala ya kashfa ya Richmond kabla ya kujiunga
rasmi na chama hicho.
“Mbona huo ushahidi aliokuja nao leo hakunishirikisha mimi kama
mwanasheria mkuu wa chama? Kwanini kaibuka leo? Na hizo gharama za
mkutano wake zimebebwa na nani?
“Tulizungumza kwenye Kamati Kuu na kabla ya Kamati Kuu ya chama, na
Lowassa akatwambia aliyeruhusu mkataba huo kuendelea ni Rais Kikwete,
Dk. Slaa alikuwepo, imeandikwa wapi kwamba lazima Lowassa alete vijana,
viongozi wangapi kutoka CCM?” alisema Lissu.
Habari zilizopatikana baadaye kutoka ndani ya Chadema zilisema licha
ya kiongozi huyo kusema aliandika barua ya kujiuzulu Julai 28 mwaka huu,
chama hicho kimeendelea kumlipa mshahara ukiwamo wa mwezi uliopita.
“Hata gari alilonunuliwa na chama ameendelea kulitumia hadi leo
(jana) ambako aliamua kulirudisha saa chache kabla ya kuzungumza na
vyombo vya habari,” kilisema chanzo hicho.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment