NYOTA wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’ anatarajia mtoto wa kiume hivi karibuni.
Prezzo amempa jina la Gabriel mtoto huyo kabla hajazaliwa. Msanii
huyo mpaka sasa hajaoa, lakini ana mtoto mmoja na sasa anatarajia kupata
mtoto wa pili.
“Natarajia mtoto wa kiume siku yoyote, ni furaha kubwa kupata mtoto
wa kiume kwa kuwa naamini ataiga mambo yangu mengi, ikiwemo aina ya
mavazi ninayopenda kuvaa.
“Nimeamua kumpa jina mapema kabla ya kuzaliwa kwa kuwa najua jinsia
yake, baada ya kufanya uchunguzi kwa madaktari,” alimaliza Prezzo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment