Mawaziri wa
fedha wa Umoja wa Ulaya wameomba ufadhili wa wakimbizi barani Ulaya kupitia kwa
bajeti huku kamisheni ya Ulaya ikikanusha pendekezo hilo wakidai kuwa
lazima sheria za kifedha lazima ziheshimiwe.
Takriban 500,000 ya wakimbizi wameingia Ulaya tangu
mwanzo wa mwaka 2015 kwa ajili ya kutoroka vita na njaa
vilivyokumba nchi zao.
Waziri wa
fedha wa Luxembourg, Pierre Gramegna alisisitiza kuwa kamisheni ya Ulaya
sharti ianzishe mbinu ya kifedha itakayosuluhisha mgogoro wa wakimbizi barani
humo.
Rais wa
kamisheni ya Ulaya Jean-Claude Juncker alipendekeza kuwahamisha wakimbizi160,000 katika nchi tofauti za bara la
Ulaya na akafanya makadirio ya gharama ya shughuli hiyo kuwa saraf ya ulaya
Euro milioni 780 sawia na dola milioni 880.
Msimamizi wa
bajeti ya Ulaya aliahidi kufanya uchunguzi wa athari za wakimbizi kwa uchumi
barani Ulaya.Hatma ya bajeti maalum kwa wakimbizi itatangazwa tarehe 5 Oktoba.
0 comments:
Post a Comment