TAMASHA
la 34 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililoanzishwa mwaka 1981 na
Chuo cha Sanaa Bagamoyo (kwa sasa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo),
linatarajiwa kufanyika kwa siku sita katika viwanja vya chuo hicho bila ya kuwa
na ushiriki wa wasanii wa Bongo Fleva.
Mwenyekiti
wa Tamasha hilo, John Mponda, alilieleza kwamba hakuna msanii wa
Bongo Fleva yeyote aliyejitokeza kuomba kushiriki katika tamasha hilo, jambo
ambalo linaonyesha kutokuwa na wasanii hao katika tamasha hilo.
“Tamasha
hilo litaanza Septemba 21 hadi 27, likiwa na kauli mbiu kwamba ‘Sanaa na
Utamaduni katika Uchaguzi huru na wa Amani’ na pia tunawakaribisha wasanii wa
bongo fleva wajitokeze kwa kuwa muda bado upo,’’ alieleza Mponda.
Mwenyekiti
huyo alisema licha ya wasanii hao kutojitokeza, lakini idadi kubwa ya vikundi
vya ngoma za asili, maigizo, sarakasi, mazingaombwe, muziki wa kisasa na asili,
sanaa za ufundi na bidhaa mbalimbali vitatoa burudani kupitia kazi zao.
Aliongeza
kwamba vikundi 48 vimethibitisha kushiriki, ambapo ni vikundi 43 vya Tanzania
na vikundi vitano kutoka nchi ya Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.
Licha ya
tamasha hilo kuwa la burudani, pia kutakuwa na mada ndogondogo zitakazotolewa
kupitia kongamano na warsha zitakazohusu haki za binadamu, rushwa na kupinga
mauaji ya albino.
Tamasha
hilo lilianzishwa ili kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo hicho kuonyesha kwa
vitendo waliyojifunza kwa mwaka mzima kwa kushirikisha wakazi wa maeneo hayo,
lakini baadaye likabadilishwa na kuwa tamasha la kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment