Rais MUHAMMAD BUHARI wa Nigeria anakwenda Ghana leo ambako atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais JOHN DRAMANI MAHAMA kujadili usalama wa ukanda huo.
Ikulu ya Nigeria imesema wakati wa ziara yake hiyo ya siku moja Bwana BUHARI ambaye juzi aliadhimisha siku 100 za kuwa madarakani pia atajadili uhusiano wa biashara na Ghana.
Bwana BUHARI aliyekuwa kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Nigeria awali alitembelea nchi
jirani za Cameroon, Chad, Niger na Benin.
Ilikuwa sehemu ya kujenga juhudi za kanda za kupambana na wapiganaji wa kikundi cha
Boko Haram tangu kuanza maasi yake mwaka 2009 kimeua zaidi ya watu 15,000 na kulazimisha wengine milioni 2.1 kukimbia makazi yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment