Image
Image

Bunge la Afrika ya Kusini limekataa kumchunguza Rais JACOB ZUMA.

Bunge la Afrika ya Kusini limekataa kumchunguza Rais JACOB ZUMA kwa ajili
ya uwezekano wa kumuondolea kinga ili ashtakiwe.
Hiyo inatokana na kumruhusu Raia OMAR al-BASHIR wa Sudan aliyekuwa Afrika ya Kusini
mwezi Juni mwaka huu akwepe hati ya kukamatwa kwake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa
ya Uhalifu ya ICC.
Bwana BASHIR anayetuhumiwa kupanga mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur aliruhusiwa
kuondoka Afrika ya Kusini kurejea nyumbani wakati mkutano wa viongozi wa Afrika
ukifanyika nchini humo.
Kuruhusiwa kwake kurejea nyumbani kulikuja kinyume na amri ya mahakama iliyokuwa
imetolewa kutaka rais huyo wa Sudan akamatwe chini ya hati ya kukamatwa kwake na
mahakama ya ICC iliyoko The Hague, Uholanzi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment