Maelfu ya wahamiaji wengine wamewasili Ugiriki wakati serikali ya nchi hiyo ikijiandaa
kwa mazungumzo ya kukabiliana na idadi kubwa ya watu wanaowasili kwenye fukwe zake.
Meli mbili zenye zaidi ya wakimbizi 4,200 zimewasili Ugiriki baada ya kutembea usiku
kucha kutoka kisiwa cha Lesbos hadi bandari ya Piraeus ya Ugiriki ambayo mwaka huu hadi
sasa wamewasili zaidi ya wahamiaji 160,000.
Hivi sasa Umoja wa Ulaya unakabiliwa na wimbi la wakimbizi ambalo halijawahi kutokea
huku mamia ya watu, wengi wao kutoka Mashariki ya Kati wakiwa bado wamekwama kituo cha
reli cha Hungary.
Wamezuiliwa kusafiri kupitia Umoja wa Ulaya na shirika la mipaka la Umoja huo, Frontex,
linasema wahamiaji 23,000 waliwasili Ugiri wiki iliyopita peke yake ikiwa ni asilimia 50
ya wiki iliyotangulia.
Home
Kimataifa
Maelfu ya wahamiaji wamewasili Ugiriki wakati serikali ya nchi hiyo ikijiandaa kwa mazungumzo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment