Image
Image

Michezo ya Commonwealth 2022 kufanyika barani Afrika.


Durban itakuwa mji wa kwanza Afrika kuwa mwenyeji wa michezo ya 'Commonwealth' mwaka 2022.

Jiji la Durban ni mojawapo ya miji iliyopo katika pwani ya Afrika Kusini.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya mkutano mkuu uliofanywa na  maafisa wa mashirika ya kufanikisha tamasha hiyo ya michezo nchini New Zealand.
Mkuu wa shirika la CGF Prince Tunku Imran alisema “Ni ufahari mkubwa kwa Afrika baada ya Durban kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo ya 22 ya Commonwealth”.

Michezo ya Commonwealth hufanyika kila baada ya miaka nne na wanariadha hutoka kwa zaidi ya nchi 50 wengi wao wakiwa raia wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.

Michezo ya Commonwealth kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 1930.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment