Chama cha NCCR mageuzi jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
kimelaani vikali kitendo cha madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo
chadema kukata kumuunga mkono mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye pia ni
mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA Bw.James Mbatia
kwa tuhuma za kusimamisha wagombea madiwani kila kata.
Akitoa taarifa kwa waandishin wa habari katibu
mwenezi wa chama cha NCCR Mageuzi jimbo la Vunjo Bw.Stanley Temba amesema
kitendo kinachofanywa na madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
ni kinyume na makubaliano kwa kuwa lengo la muungano wa vyama hivyo ni kupata
ushindi kuanzian ngazi za chini hadi urais
Amesema mgawanyiko huo utaasababisha wananchi kukosa
imani na viongozi wa vyama vinavyounda ukawa na kwamba ni vema madiwani hao
wakaacha hasira badala yake kukaa pamoja na kujadiliana ili kuondoa
kasoro zilizojitokeza badala ya kumsusia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa
tiketi ya NCCR Bw.James Mbatia.
Naye mjumbe wa halimashauri kuu wa chama cha NCCR Mageuzi
taifa Bw.Hemed Msabaha amekiri kuwa chama hicho kimesimmisha wagombea udiwani
katika kata zote kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho ndiyo wanakubalika
zaidi katika jamii ikilinganishwa na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.
Hata hivyo juhudu za kuwapata viongozi wa chama cha
demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa kilimanjaro kuzungumzia sakata hilo
zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment