Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiongoza kikao kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wa pili kulia akifafanua jambo wakati kikao kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.
Baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Mafunzo kwa Mtandao(TaGLA), Charles Senkondo akifafanua jambo kuhusu matumizi ya njia ya video leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo jijini Dares Salaam.
Serikali imefanikiwa kuboresha utendaji
kazi wa utumishi wa umma kwa kuendesha mikutano kupitia njia ya video(TEHAMA)
katika taasisi zake,wizara idara ili kuongeza kwa ufanisi na tija kwa gharama
nafuu kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwa muda mfupi.
Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu
wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uendeshaji wa kikao
kazi kupitia njia ya video kwa makatibu tawala wa mikoa na wasaidizi
wao, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa idara za utawala
na rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa kwenye mikoa ya
Dares Salaam, Kagera, Tanga,Tabora,Manyara, Morogoro, Rukwa na Katavi
kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Wakala wa Mafunzo kwa Mtandao iliyopo
jijini Dares Salaam.
“Serikali imebuni sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao
katika kutekeleza majukumu yetu kwa kulenga tija na ufanisi. Leo tunazungumzia mpango
wa Matokeo Mkubwa Sasa (BRN) ili tupate matokeo ya BRN kwa
ufanisi na kwa wakati hatuna budi kutumia TEHAMA,” alisema Kaimu
Katibu Mkuu huyo.
Mkwizu alisema mkutano huo ni wa awamu
ya kwanza kufanyika kwa kupitia njia hiyo, hivyo vikao vitatu
vimefanyika, kikao cha kwanza kufanyika kilifanyika Septemba
15,mwaka huu ambao ulihusisha watendaji hao kwenye mikoa ya Mwanza, Mbeya,
Kilimanjaro, Dodoma , Ruvuma Kigoma,Lindi na Geita.
Aliongeza kwamba mkutano wa awamu ya pili ulifanyika
Septemba 17, mwaka huu ambapo ulihusisha watendaji hao kwenye mikoa ya Arusha,
Singida,Pwani,Iringa, Mara,Mtwara, Shinyanga, Njombe na Simiyu.
Alizitaja mada zilizojadiliwa
katika mikutano hiyo kuwa ni Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka
2010 na kanuni zake, wajibu wa waajiri katika ufuatiliaji na uzingatiaji wa
maadili katika utumishi wa umma , ukaguzi wa rasilimali watu katika utumishi wa
umma, ambalo ni jukumu la msingi la Tume ya Utumishi wa Umma,ambao
wanakagua mifumo yamenejimmenti rasilimali watu ya utumishi wa umma
na kuona inatekelezwa vipi na tathimini ya kazi katika utumishi wa
umma ili kulinganisha kazi mbalimbali na hatimaye kuja na mapendekezo kazi
mbalimbali watu walipwe vipi kulingana na unyeti, madaraka ili zinazofanana
zilipwe sawa na zisizofanana zilipwe tofauti.
Alisema awamu ya pili ya uendeshaji wa mikutano kwa
kutumia njia hiyo itafanyika Novemba mwaka huu.
Mkwizu alifafanua kwamba tayari Serikali imeshaweka
mwongozo katika taasisi zake na mamlaka za Serikali ili ziweze kufanya mikutano
au kikao kazi kwa njia video. Hivyo mikoa yote imeshafungiwa vifaa maalum kwa
ajili ya matumizi hayo isipokuwa mikoa mipya ambayo ambayo hujiunga na mikoa
mama.
Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa Wakala
wa Mafunzo wa Serikali Mtandao(TaGLA), Charles Senkondo alisema ulianzishwa
mwaka 2011 ili kuongeza kasi ya uboreshaji wa huduma.
Alisema mfumo huo umewezesha madaktari bingwa
wa hapa nchini kuweza kutibu wagonjwa kwa kuwasiliana na madaktari wenzao
mabingwa kutoka nje ya nchi, watu kufanya usaili na kupata kazi za kimataifa na
mahakama kuendesha kesi kwa kuwasiliana na mashahidi walioko nje ya
nchi.
Alizitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni
pamoja na baadhi ya watu kuwa na fikra potofu katika matumizi ya
TEHAMA, wengine wanafikiri ni kitu kigumu na kuwa na woga wa kutumia
lakini kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau
mbalimbali wameendesha mikutano mingi na wanao uwezo wa kutoa
ushauri na mwongozo inayosaidia kuendesha mikutano kupitia njia hiyo ili iweze
kufanyika vizuri.
"Watanzania wafahamu kwamba wakala wa mafunzo
kwa njia ya mtandao imeanzishwa na Serikali kwa ajili yao, hivyo ninatoa wito
waweze kuitumia na kupeleka taarifa kwa urahisi ambazo zinawafikia
watu wengi kwa wakati mmoja na sisi tuko tayari kutoa ushauri ili
mikutano kufanyika ipasavyo", alisema Senkondo.
0 comments:
Post a Comment