Watu wa tano wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA- waliokuwa wamekamatwa na kufikishwa mahakani wakidaiwa kupanga njama za uvunjifu wa amani na kuvuruga mchakato wa uchaguzi katika Kata ya Muhutwe Jimbo la Muleba Kaskazini na kukaa mahabusu kwa siku kadhaa bila kupewa dhamana wamefanikiwa kupata dhamana na kuendelea na shughuli zao za siasa.
Watuhumiwa
hao waliokamatwa ni pamoja na mgombea Udiwani Kata ya Muhutwe, ELIEZA
LUHIPULA pamoja na wafuasi wake wanatuhimiwa kwa kufanya njama za
uvunjifu wa amani katika harakati za kampeni.
Akizungumza
katika mahakama hiyo Mwendesha Mashitaka wa Polisi CHARLES MPELWA
amesema mahakama ilizuia kutoa dhamana kwa washitakiwa hao kwa siku
kadhaa kutokana na kesi yao inayohusu upangaji wa njama za uvunjifu wa
amani.
Hata
hivyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Muleba, BENEDICT NKOMORA
ameamuru kuwa kila mshitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa dhamana ya
Shilingi Laki-mbili mpka siku ya tarehe kumi na sita mwezi novemba
watakapo rejea tena mahakamani hapo .
0 comments:
Post a Comment