Jenerali aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso huko Afrika ya Magharibi amesema yuko
tayari kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kama ilivyopendekezwa na wapatanishi wa
Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS.
Jenerali GILBERT DIENDERE pia ameomba radhi kwa taifa hilo na kusema kuwa alichukua
hatua hiyo kwa lengo la kuzuia umwagaji mkubwa wa damu.
Kauli yake inakuja huku majeshi ya serikali yakiwa yameingia mji mkuu wa nchi hiyo,
Ouagadougou na kuahidi kutowaangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo tu watasalimisha
silaha zao.
Jenerali huyo kwa sasa anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi mmoja wa jadi.

0 comments:
Post a Comment