Image
Image

Mutungi awataka viongozi dini,wamiliki wa vyombo vya habari na asasi za kiraia kutumiwa na wanasiasa.

Msajili wa vyama vya siasa nchini Mh.Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa mathehebu ya dini,wamiliki wa vyombo vya habari na asasi za kiraia wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani iliyodumu miaka 54 ya uhuru wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Wito huo umetolewa jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya amani duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza na kuhususha, viongozi wa madhehebu ya dini, asasi za kiiraia, wasomi, walemavu, wamiliki wa vyombo vya habari na wandishi wa habari Mh.Jaji Mutungi amesema kuwa siasa ya Tanzania inatumika vibaya hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani endapo isipodhibitiwa kwa wakati.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na utoaji elimu, sayansi na utamaduni kwa jamii UNESCO nchini Tanzani Bi.Zurmila Rodriguez amewataka watanzania kudumisha amani iliyopo miaka 54 ya uhuru hasa kwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 kwa kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambaye alipigania ukombzi wa nchi za Afrika na kuitangaza Tanzania kuwa kisiwa cha amani duniani.
Kwa upandewake kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza mchungaji Baraka Konisaga amesikitishwa na vurugu za wananchi kuchukua sheria mikononi kwa kuvunja gari la jeshi la polisi vioo ambapo naibu kamishina wa polisi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkubo ameuhakikishia umoja wa mataifa kuwa jeshi la polisi Tanzania limejipanga kikamilifu kuimalisha ulinzi wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura na siku ya kutangaza matokeo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment