Kiongozi wa zamani wa Chad Bwana HISSENE HABRE amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuamuru mauaji ya watu 40,000 wakati wa enzi ya utawala wake katika miaka ya themanini,madai ambayo amekanusha.
Wakati wa kuanza kesi yake ya uhalifu wa kivita rais huyo wa zamani wa Chad alishikiliwa
na maafisa wa usalama waliofunika nyuso zao na alilazimisha kwenda mahakamani baada ya
kukataa kuhudhuria.
Kesi yake inaweka rekodi ya kwanza ya nchi moja ya Afrika kummshitaki kiongozi wa nchi
nyingine na Bwana HABRE amekataa kutambua uhalali wa mahakama inayoendesha kesi yake.
Mahakama hiyo maalum iliundwa na Umoja wa Afrika mwaka 2013.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment