Shirika
hilo limesema kwamba litaweza kutekeleza safari za ndege 500 pekee kati
ya 1,520 zilizokuwa zimepangwa siku ya Jumatano kufuatia mgomo wa
marubani ulioanza siku ya Jumanne.
Maelezo
zaidi yanaarifu kwamba takriban wasafiri 140,000 wameathiriwa na uamuzi
huo uliosababishwa na mgomo wa marubani.
Hata
hivyo, shirika la Lufthansa limetangaza kwamba shughuli za usafiri kwa
washirika wake kama vile Germanwings, Swiss, Austrian Airlines na Brussels
Airlines zitaendelea kama kawaida.
Siku
ya Jumanne, shirika la Lufthansa lililazimika kufutilia mbali safari
za ndege 84 kati ya 170 zilizokuwa zimepangwa kuelekea katika miji
ya Frankfurt, Munich na Duesseldorf.



0 comments:
Post a Comment