Image
Image

Ndege moja ya British Airways aina ya Boeing 777 yawaka moto wakati wa kuruka mjini Las Vegas.


Ndege moja aina ya Boeing 777 ya shirika la Uingereza la British Airways, imeripotiwa kuwaka moto hapo jana wakati ilipokuwa ikitaka kuruka katika mji wa Las Vegas.
Ndege hiyo yenye safari za nambari ya 2276, ilikuwa imepangiwa kuanza msafara wake wa kuelekea katika uwanja wa ndege wa Gatwick ulioko London nyakati za jioni.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na maafisa wa utawala wa uwanja wa ndege wa McCarran ulioko Las Vegas, ndege hiyo iliwaka moto katika upande wa mitambo ilipokuwa ikitaka kuruka.
Baada ya tukio hilo, marubani na wafanyakazi wa ndege hiyo walilazimika kusitisha safari na kutoa abiria wote waliokuwemo ndani.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 yenye viti 275, ilikuwa imebeba abiria 159 pamoja na wafanyakazi 13.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba abiria wawili walipata majeraha madogo yanayofanyiwa matibabu.
Chanzo cha kuzuka kwa moto huo bado hakijabainika ingawa picha za video zilizonaswa na kamera za uwanja wa ndege wa McCarran zinazoonesha wingu la moshi mweusi likitokea katika upande wa kushoto wa mitambo ya ndege.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment