Tume ya uchaguzi ya Morocco imetangaza kukamatwa kwa watu 46 kwa madai ya ukiukaji wa sheria wakati wa uchaguzi wa serikali za manispaa uliofanyika siku ya Ijumaa nchini Morocco.
Tume hiyo iliarifu kuchunguza kesi 1,240 zilizoripotiwa wakati wa uchaguzi, zinazojumuisha kesi 831 zinazozuka katika kipindi cha kampeni na kesi 339 zilizotokea wakati wa kupiga na kuhesabu kura.
Licha ya madai hayo kutolewa, tume hiyo imebainisha kukamilishwa kwa shughuli ya uchaguzi katika misingi ya kisheria na haki.
Wakati wa uchaguzi huo, jumla ya wawakilishi 4,000 wakiwemo 76 kutoka mashirika ya kimataifa walifuatilia makini shughuli ya upigaji kura.


0 comments:
Post a Comment