Polisi nchini Kenya wamewatiwa mbaroni watu 3 hapo jana waliokuwa na vilipuzi katika jengo la biashara la Garden City Mall lililoko viungani mwa jiji la Nairobi.
Kamanda wa polisi wa eneo la Kasarani Robin Mboloi, alisema kwamba walinzi wa Garden City Mall waligundua vilipuzi hivyo baada ya kufanya ukaguzi mlangoni.
Baadaye walinzi waliwazuia watu hao na kutoa ripoti kwa polisi ambao waliwasili mara hiyo hiyo na kuwatia mbaroni.
Tukio hilo lilizua hali ya mtafaruku miongoni mwa watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo la biashara.
Mboloi pia alisema kwamba wataalamu wa kutegua mabomu waliwasili na kutaifisha vilipuzi hivyo vinavyodaiwa kuwa na uwezo wa kusababisha hasara kubwa.
Jengo la biashara la Garden City Mall lililokuwa na maduka ya wafanyabiashara wa ndani ya nchi na kimataifa, lilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai jijini Nairobi.


0 comments:
Post a Comment