Image
Image

Magufuli:Sitaendesha nchi kidikteta kama baadhi ya watu wanavyodai.

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano,hataendesha nchi kidikteta kama baadhi ya watu wanavyodai.
Amesema atazingatia sheria za nchi lakini hatakuwa na simile kwa watu watakaoleta mchezo kusimamia rasilimali za nchi.
Dk.Magufuli alitoa kauli hiyomjini Chato jana alipohutubia maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo. Alisema ili nchi iweze kusonga mbele inahitaji mtu ambaye hajui kesho ila ni harakaharaka kutatua kero za wananchi.
“Ninajua hapa Chato kuna mkandarasi amepewa mradi wa maji haendi kwa kasi, sasa akamilishe haraka maana Oktoba 25, nikichaguliwaeheee…
“Mimi ninachojua ni harakaharaka na si polepole kuhakikisha Watanzania wanapatiwa huduma kwa wakati, watu wa aina hii sasa waanze kujirekebisha mapema.
“…nitaendesha Serikali kwautaratibu na siyo kidikteta, nitafuata sheria kuna watu wanasema mimi ni mkali ila wajue kwanza ni kazi tu… jukumu langu ni kuhakikisha watu wa chini wananufaika na rasilimali za Serikali yao na nchi yao,” alisema Dk. Magufuli Alisema amejiandaa kujenga Tanzania mpya ya viwanda ambavyo vitasaidia kujenga uchumi na ajira kwa vijana.
Alisema ili nchi iweze kuendelea inahitaji kuwa na viwanda vya uhakika na Serikali yake ya awamu ya tano italitekeleza suala hilo kwa vitendo.
Alisema amegombea nafasi ya urais si kwa majaribio bali anataka awafanyie kazi Watanzania ambao wanataka
mabadiliko.
Alisema mabadiliko ya kweli yanaweza kutokea, hakuna budi kwa Serikali yake ilifanye suala hilo kama kipaumbele chake.
“Kila awamu ilifanya kazi, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (Julius) alileta umoja na amani kwa Watanzania, akaja mzee Mwinyi (Ali Hassan), mzee Mkapa (Banjamin) na hata Rais Jakaya Kikwete alifuata misingi hiyo sambamba na maendeleo ya nchi yetu.
“Hata Waziri Mkuu mmoja mstaafu ametajwa hapa (Sumaye), amekaa Hanang’ miaka 10 hakuna hata lami, ameondoka tumejenga lami kilometa zaidi ya 80 huyo ndiyo Magufuli, kwangu ni kazi tu pamoja na yeye kusema CCM haijafanya kitu,” alisema Dk. Magufuli
Wafanyakazi
Alisema Serikali yake itawalipa mishahara mizuri wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuboresha masilahi yao ya
mishahara na fedha za likizo kwa wakati.
Dk. Mgufuli alisema yeye ni rafiki wa wafanyakazi ambao wamekuwa wakichangia mapato kila mwezi jambo ambalo
limekuwa likiwaumiza.
Alisema atahakikisha Serikali yake inapunguza kodi kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo kuinua uchumi wao.
“Mimi ni rafiki wa wafanyakazi na hili liko wazi ndiyo maana hata nikiwa Waziri wa Ujenzi nimeongoza wakala (agency) ya Wakala wa Barabara Tanzania(Tanroads), ambayo inafanya kazi kubwa.
“Imefika mahali kwa watumishi wake kulipwa hadi Sh milioni tisa kwa mwezi na wala sichukii kwa sababu  wanafanya kazi.
“Ni hili tutaendelea nalo hata nitakapokuwa rais… ikiwa mtanichagua masilahi ya wafanyakazi yatakuwa mazuri tu.Tutapunguza kodi na kuongeza masilahi bora zaidi ili wafanye kazi kwelikweli,” alisema Dk. Magufuli
Alisema anajua kuna kikundi cha watu wachache ambao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watendaji kumiliki rasilimali za nchi.
Mke wake
Jana ilikuwa mara ya kwanza kwa mke wa Dk.Magufuli, Janeth Magufuli, kusimama kwenye jukwaa na kumuombea
kura mume wake.
Alisema Dk. Magufili amekuwa mbunge kwa miaka 20 hivyo anatosha kuaminiwa na Watanzania kuwa rais.
Alisema kutokana na hali hiyo anajua jinsi Watanzania wanavyomuamini mume wake na ndiyo maana Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kimemteua kugombea urais.
“Chato mmetutia moyo, mmempa heshima kubwa Dk. Magufuli kwa kumchagua kama mbunge wenu miaka 20,asanteni.
Bulembo
Akizungumza katika mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni, Abdallah Bulembo, alisema anashangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutaka CCM ipelekwe Mahakama ya
Uhalifu ya Kimataifa (ICC).
“Mbowe anahoji Bulembo ni nani, ninamwambia nilianzia chipukizi, UVCCM, nimekuwa diwani kwa miaka 16 sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu… sikuingia kwa bahati mbaya CCM,” alisema Bulembo
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment