Image
Image

Mahakama ya Kenya yasimamisha agizo la serikali kutaka shule za binafsi zifungwe.

Mahakama ya Kenya imesimamisha agizo la serikali kutaka shule za binafsi pia zifungwe
pamoja na zile za umma kutokana na mgomo wa walimu na hivyo kuleta ahueni kwa shule
binafsi.
Agizo hilo linafuatia kesi iliyowasilishwa na Chama cha Shule za Kibinafsi kupinga agizo
la wizara ya elimu lililotolewa Ijumaa wiki iliyopita.
Serikali ya Kenya iliagiza kuanzia jana wanafunzi wote wabaki nyumbani isipokuwa wale tu
wanaojiandaa kwa mitihani ya kitaifa.
Lakini mahakama ilisitisha agizo hilo upande wa shule za kibinafsi kwa siku tatu
kusubiri kusikizwa kwa kesi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment