Ijumaa iliyopita mahujaji 107 waliokuwa wakisali
katika Msikiti wa Makka walikufa na wengine kujeruhiwa baada kuangukiwa na
ukuta ulioanguswa na winchi iliyokuwa jirani msikiti huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu
alisema Baraza la Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wanafuatilia kwa karibu ili
kujua hali ya mahujaji hao.
“Tunafuatilia ili kufahamu usalama wa mahujaji wetu
na tutakuwa tunatoa taarifa za maendeleo ya tukio hilo kila tutakapopata
taarifa,” alisema.
Alisema kwa sasa baraza hilo halina idadi ya
mahujaji waliokwenda kuhiji kwani kuna wengine walishaondoka Septemba 9 mwaka
huu na wengine wanaendelea kwenda huko.
“Hili ni tukio la kusikitisha na ni msiba mkubwa
kwetu, sisi waislamu kila tunapopata msiba huwa tunasema sisi sote tunatoka kwa
mwenyezi Mungu na kwake tutarejea,” alisema.
Alitoa wito kwa misikiti yote nchini kuwaombea dua
waliotangulia mbele ya haki na kwamba Mungu awasamehe madhambi yao.
“Nawaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa watulivu
na kumwomba Mungu ili warejee wakiwa salama,” alisema.
0 comments:
Post a Comment