Umoja wa mataifa umeelezea
masikitiko yake dhidi ya mataifa kadhaa ya bara Ulaya, ya namna
yanavyozingatia sheria mbalimbali zinazokinzana kuhusiana na mipaka
yake.
Shirika linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, linaonya kuwa
hatua hii itawaacha maelfu ya wakimbizi katika hali ya kutatanika
kisheria.
Shirika hilo la UNHCR, linasema kwamba muungano wa bara
Ulaya, unafaa kubuni vituo vya kuwapokea wahamiaji, kuwaandikisha na
kuwapiga msasa wahamiaji na wale wanaotafuta makao huko hasa wanaowasili
nchini Ugiriki, Italia, na Hungary.
Kupitia taarifa kabla ya kufanyika kwa mkutano unaowaleta pamoja
mawaziri wa haki na sheria wa muungano wa ulaya hatimaye leo Jumatatu,
shirika hilo linasema kuwa mataifa ya bara Ulaya yanahitajika
kuharakisha kubuni taratibu au sheria ya kushughulikia mpango huo wa
wahamiaji.
Mataifa ya Ujerumani, Austria na Jamhuri ya Czech
yametoa ulinzi mkali katika mipaka yao. Ujerumani inasema kuwa,
imetamaushwa na ongezeko la wahamiaji wanaoingia nchini humo.
Takriban wahamiaji elfu 16 waliingia katika mji wa Munich pekee, mwishoni mwa juma.
0 comments:
Post a Comment