Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameripotiwa akisema kuwa anashtumiwa bila ushahidi wa makosa aliyofanya.
Matamshi
yake yanajiri wakati alipoitwa 'mnafiki na muongo' na Chung Mong-Joon
ambaye anapanga kumshataki raia huyo wa Uswizi kwa ubadhirifu wa fedha
huku vilevile akitaka kumrithi katika FIFA.
Blatter anakabiliwa na uchunguzi kwa tuhuma za kutekeleza uhalifu wakati wa uongozi wake katika FIFA.
'Hakuna mashtaka',raia huyo mwenye umri wa miaka 79 aliliambia jarida moja la Ujerumani Bunte.
Blatter ambaye atastaafu mnamo tarehe 26 mwezi Februari ,aliongezea:''Huu ni uchunguzi tu''.
''Nitapigana hadi mwezi Februari ,kwa haki yangu na ile ya FIFA,Ninahakika kuwa uovu huo utabainika mwishowe''.
Aliyekuwa
makamu wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Chung alifichua wiki
hii kwamba anachunguzwa na kamati ya maadili ya FIFA na kusema kuwa
hatua hiyo imekandamiza kampeni ya uongozi wake.
0 comments:
Post a Comment