Shirika la umeme Tanzania -Tanesco limesema hali ni mbaya ya upatikanaji wa umeme nchini kutokana na chanzo kikuu ambacho ni mabwawa ya kuzalishia nishati hiyo asilimia 18 tu ya uwezo wake.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo mhandisi Felchesm Mramba amewaambia waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kuwa makali ya tatizo hilo yamewafanya washindwe kuita kukosekana huko umeme nchini kama ni mgawo au dharura.
Hata Hivyo Mhandisi Mramba amesema kwa kiasi fulani yamepunguzwa kutokana na kupatikana kwa nishati ya gesi ambapo pia jumanne ya wiki hii wamefanikiwa kuwasha megawati 30 kutoka kampuni ya simbioni.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dar Es Salaamm wameiomba Serikali kuibana Tanesco na kueleza kukosekana huko kwa umeme kunakoendelea sasa hapa nchini kutamalizika lini.
0 comments:
Post a Comment