Wananchi wa jimbo la Mvomero pamoja
na Gairo mkoani Morogoro wamemuomba rais ajaye kuhakikisha anashughulikia kero
zao mbalimbali, ikiwemo ya wakulima wa mahindi na miwa kuchukuliwa mashamba yao
na wawekezaji wakubwa bila fidia stahiki na kushindwa kufanya kilimo pamoja na
kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikisababisha
mauaji ya raia na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya mkoa wa Morogoro
Mgombea mwenza wa urais wa jamhuri
ya muungano wa tanzania kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA
), anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ),Mh.Juma
Duni Haji anawasili katika kata ya hembeti jimbo la mvomero na magore jimbo la
kilosa kati na kulakiwa kwa orodha ndefu ya kero za wananchi.
Mgombea ubunge wa jimbo la Gairo
kupitia Chadema Salum Mpanda anasema akipewa ridhaa na wananchi ya kuingia Bungeni
atafuta michango yote ya shule ambayo ni kero kwa wazazi na kutumia vyanzo
vingine vya mapato kuboresha huduma za kijamii.
Ikafika zamu ya mgombea mwenza
Mh.Juma Duni Haji kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
shule ya msingi gairo,jimbo la gairo na ujumbe wake hapa ukalenga zaidi kuwatia
hamasa wananchi kwa ajili ya kwenda kupiga kura tarehe 25 mwezi huu ili kufanya
mabadiliko kwa kuiondoa madarakani serikali ya chama cha mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment