KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa, amewahakikishia Watanzania mabadiliko
makubwa wakati timu hiyo itakapomenyana na Malawi leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars itakuwa mwenyeji wa Malawi katika mchezo wa hatua ya awali ya mtoano wa mashindano ya kuwania kufuzu
Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Stars chini ya Mkwasa haijaambulia ushindi kwenye mechi tatu zilizopita alizoanza kuinoa timu hiyo, akianza kwa
kutoa sare dhidi ya Uganda (1-1), akafungwa na Libya (2-1) kwenye mechi ya kirafiki kabla ya kutoa suluhu na Nigeria.
kutoa sare dhidi ya Uganda (1-1), akafungwa na Libya (2-1) kwenye mechi ya kirafiki kabla ya kutoa suluhu na Nigeria.
Mkwasa ataingia kwenye mchezo huo akiwa na morali kubwa baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumpa
mkataba wa kudumu wa mwaka mmoja na nusu kuinoa timu hiyo unaoanzia Oktoba Mosi, mwaka huu hadi Machi 31, 2017.
mkataba wa kudumu wa mwaka mmoja na nusu kuinoa timu hiyo unaoanzia Oktoba Mosi, mwaka huu hadi Machi 31, 2017.
Mkataba huo unamwezesha Mkwasa kupata huduma zote na marupurupu
aliyokuwa akipewa mtangulizi wake Mholanzi, Mart Nooij, aliyetimuliwa
kutokana na matokeo mabaya, ikiwemo nyumba, gari na mshahara wa Sh
milioni 25 kwa mwezi, sawa na Dola za Kimarekani 12,500.
milioni 25 kwa mwezi, sawa na Dola za Kimarekani 12,500.
Mkwasa, aliyefurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa na TFF, ataweza
kuvuna kiasi cha Sh mil 450 kwa kipindi cha miezi 18 ya mkataba huo,
huku akiahidi kufanya jitihada kuongeza kiwango cha Stars.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkwasa alisema mchezo huo utakuwa mgumu, lakini wamejiandaa kupambana ili
kuibuka na ushindi nyumbani, huku akisisitiza dakika 90 zinatosha kuleta mabadiliko ya soka nchini.
kuibuka na ushindi nyumbani, huku akisisitiza dakika 90 zinatosha kuleta mabadiliko ya soka nchini.
“Dakika 90 zitaweza kuleta mabadiliko na kutupatia ushindi ambao ni
muhimu kwetu, kwani ninawafahamu vizuri Malawi kwa kuwa soka lao halina
tofauti na kwetu,” alisema.
Stars itaingia dimbani ikichagizwa na moto wa washambuliaji wake wa
kulipwa, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, waliofanya vizuri kwa siku
za hivi karibuni wakiwa na TP Mazembe, iliyotinga fainali ya Ligi
ya MMabingwa Afrika, pamoja na Mrisho Ngassa aliyeanza kung’ara akiwa Free States Stars ya Afrika Kusini.
ya MMabingwa Afrika, pamoja na Mrisho Ngassa aliyeanza kung’ara akiwa Free States Stars ya Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment