Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki
dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na
rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya
ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina hayajapatikana
mara moja.
Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa. Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.

0 comments:
Post a Comment