Spika wa bunge la Tanzania Bi. Anna Makinda amesema kuwa Marehemu Deo
Filikunjombe, alikuwa ni mbunge wa tofauti kutokana na alivyo kuwa
akifanyakazi zake kwa kuwajali zaidi wananchi wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika mazishi ya Mbunge huyo Spika Makinda
amesema kuwa Filikunjombe alikuwa ni mpiganaji kwa kufanya kile
anachokiamini na kuikosoa serikali pindi inapokwenda tofauti pamoja na
huhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Amesema kuwa wananchi wamempoteza mpigania haki zao na wakakikishe
kuwa wanaangalia mbunge atakeye kuwa tayari kumalizia mipango aliyokuwa
ameianza mbunge huyo.
Aidha kwa upande wake Rafiki yake mpendwa wa Fili kunjombe, Kiongozi
wa Chama cha ACT wazalendo, Zito Kabwe, amesema kuwa anasikitika kutokea
kwa msiba wa rafiki yake huyo na kuwa hatoweza kumpata rafiki wa aina
ya Filikunjombe kutokan ana alivyokuwa.
Amesema kuwa kwa wakazi wa Ludewa wamempoteza mtu muhimu sana na kuwa
hawatampata mbunge kama huyo licha ya kuwa watapata mbunge lakini
hawezi kufanana na Deo.
Akihubiri katika ibada ya mwisho ya msiba wa marehemu watatu ambao
ibada ilikuwa ni moja Askofi wa Kanisa la Romani Katoliki jimbo la
Njombe, ask. Alfred Maluma alisema kuwa msiba huo ni mkubwa kwa kuwa
umehusisha watu watatu wanaotokea sehemu moja na kuwatia moyo wafiwa kwa
kuwaambia kuwa wawe wavumilivu katika siku hizi ngumu kutokana na msiba
wenyewe ulivyotokea na ughafla wake.
Katika msiba huo kuna viongozi mbalimbali walifika kuomboleza akiwemo
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi, Waziri wa maliasili na
Utalii Lazaro Nyarandu, Wiliamu Lukuvi, na viongozi wengine wa chama cha
mapinduzi wa nyazifa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment