Umoja wa Ulaya na Uturuki zimekubaliana kushirikiana katika
kuushughulikia mgogoro wa wakimbizi. Rais wa Halmashauri ya Umoja wa
Ulaya alifahamaisha hayo baada ya mkutano uliofanyika mjini Brussels
Umoja wa Ulaya na Uturuki zimekubaliana juu hatua ya kuwazuia wakimbizi kuingia katika nchi za Umoja huo.
Kulingana na mapatano yaliyofikiwa, Uturuki imekubali kuwakabili watu
wanaowasafirisha wakimbizi kwa njia za kihalifu na pia imekubali
kuwaweka nchini mwake wakimbizi zaidi, kati ya mamilioni wanaowasili
nchini humo kutoka Syria.
Makubaliano hayo yalifikiwa kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi
za Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels hadi leo alfajiri .
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker ameeleza kwamba
taarifa ilipatikana mapema leo juu ya kufikiwa makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki. Ameeleza kwamba mpango wa pamoja uliokubaliwa unalenga shabaha mbili.Kwanza kuhakikisha kwamba wakimbizi walioko nchini Uturuki wanabakia katika nchi hiyo "
taarifa ilipatikana mapema leo juu ya kufikiwa makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki. Ameeleza kwamba mpango wa pamoja uliokubaliwa unalenga shabaha mbili.Kwanza kuhakikisha kwamba wakimbizi walioko nchini Uturuki wanabakia katika nchi hiyo "
Bwana Juncker amesema lengo la pili la mpango wa pamoja baina ya Umoja
wa Ulaya na Uturuki ni kuwazuia wakimbizi na wahamiaji kuingia Ulaya kwa
kupitia Uturuki.
Uturuki kupewa fedha zaidi
Kulingana na mpango huo wa pamoja viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubali
kuipa Uturuki fedha , kiasi cha Euro Bilioni 3 ili iweze kuwahudumia
wakimbizi walioko katika nchi hiyo kutoka Syria na pia wamekubali
kuuharakisha mchakato wa kulegeza masharti ya kupata vibali kwa wananchi
wa Uturuki wanaotaka kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya.
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema makubaliano
yaliyofikiwa na Uturuki ni hatua muhimu lakini amesema makubaliano hayo
yanapaswa kutekelezwa.
Amesema maamuzi muhimu yaliyopitishwa yatasaidia katika juhudi za
kuidhibiti mipaka ya Umoja wa Ulaya. Bwana Tusk ameunga mkono
makubaliano juu ya mpango wa pamoja baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki
wenye lengo la kuishughulikia mizizi ya tatizo la ukimbizi.
Uturuki ndicho kituo muhimu cha kwanza kilichotumiwa na wakimbizi
600,000 walioingia barani Ulaya mnamo mwaka huu.Wengi wao wametumia njia
za mkato ambazo ni za hatari.
Mkimbizi apigwa risasi na kufa
Hata hivyo mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya ulifanyika katika
mukhtadha wa kifo cha mkimbizi mmoja kutoka Afghanistan aliepigwa risasi
na walinzi wa mpakani wa Bulgaria, wakati akijaribu kuingia Ulaya
kutokea Uturuki.Bulgaria imeweka polisi na wanajeshi 2000 kwenye mpaka
wake na Uturuki.
Kwa mujibu wa taarifa mtu huyo alipigwa risasi wakati kundi kubwa la
wakimbizi lilipokuwa linajaribu kuvuka mpaka. Mtu mwengine pia
alijeruhiwa kwa kupigwa risasi. Waziri wa mambo ndani wa Bulgaria
amesema wakimbizi 50 kutoka Afghanistan walisimamishwa na walinzi wa
mpakani walipokuwa wanajaribu kuvuka mpaka.
Watu 3000 wameshakufa mnamo mwaka huu tangu mgogoro wa wakimbizi
uanze.Wengi wamekufa maji wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania
ili kuingia Ulaya.
Mkataba baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki ulifikiwa baada ya wajumbe wa
Halmashauri ya Umoja huo kufanya ziara nchini Uturuki katika jitihada
za mwisho za kuishawishi serikali ya nchi hiyo kutia saini makubaliano.
0 comments:
Post a Comment