Saudi Arabia na waitifaki wake wanaoendelea kuishambulia Yemen wanazidi
kuzuia misaada muhimu ya kibinadamu kuwafikia raia wasio na hatia wa
nchi hiyo.
Kanali ya televisheni ya al-Alam imeripoti leo kwamba,
manowari za kivita za Saudia na nchi waitifaki zimezuia meli za
kibiashara zinazobeba misaada ya kibinadamu kutia nanga katika bandari
za Yemen. Meli hizo zenye misaada ya chakula na dawa zimeshindwa kufika
Yemen kutokana na nchi hiyo kuzingirwa kila kona na muungano wa Waarabu
unaoongozwa na Saudi Arabia.
Huku hayo yakijiri, jeshi la Yemen
likisaidiwa na wapiganaji wa harakati ya wananchi ya Ansarullah,
limefanikiwa kuwaangamiza wanajeshi kadhaa wa Saudia katika eneo la
mpakani. Jeshi la Yemen na mahouthi wamevurumisha makombora kuelekea
Saudi Arabia kama njia ya kujibu mapigo mashambulizi ya anga ya Riyadh
na waitifaki wake dhidi ya raia wa Yemen hususan wanawake na watoto.
0 comments:
Post a Comment